SIRI ZA BIBLIA: NGUVU ZA MADHABAHU/MAAGANO NA MIKATABA YA KUZIMU
Manage episode 313499878 series 3273506
MAMBO MUHIMU YANAYOUNDA MADHABAHU
Ili uweze kushughulikia tatizo sugu lililoshikiliwa kwenye madhabahu ni lazima ufahamu vizuri kuwa madhabahu sio jina pekee bali ni muunganiko wa mambo sita (6) ambayo hayo yanafanya madhabahu kuwepo na kuwa na nguvu, mambo hayo ni kama yafuatayo:-
Madhabahu yenyewe
Kuhani wa madhabahu
Kafara ya madhabahu
Washirika wa madhabahu
Mungu wa madhabahu
Nguvu ya madhabahu
Madhabahu yenyewe
Madhabahu hujengwa na watu kwa kusudi la kufanya ibada kwa Mungu wanaye mwamini. Kwa kawaida kila mwanadamuanaamini kuwepo kwa nguvu ambayo ni kubwa kuliko nguvu ya kibinadamu (existence of super natural power). Ili kuwasiliana na nguvu hii mwanadamu inambidi kutengeneza utaratibu wa kuifikia nguvu hiyo (kujenga madhabahu). Iwe ni kwa upande wa nuru au giza madhabahu lazima ijengwe kwa jinsi ya mwili kabisa. Eliya alijenga madhabahu ya Bwana (1Wafalme 18: 32 “Naye akaijenga madhabahu kwa mawe hayo katika jina la Bwana; akafanya mfereji, kama wa vipimo viwili vya mbegu, ukiizunguka madhabahu”)
Vilevile makuhani wa shetani nao hujenga madhabahu 1Wafalme 16:33 “Ahabu akaifanya Ashera; Ahabu akazidi kumghadhibisha Bwana, Mungu wa Israeli, kuliko wafalme wote wa Israeli waliomtangulia.”
Ninachotaka ufahamu hapa ni kwamba madhabahu hujengwa kwa jinsi ya mwilini iwe ya Jehova au ya miungu.
Kuhani wa madhabahu
Kuhani wa madhabahu ni mtu anayejua taratibu za madhabahu na mwenye uwezo(nafasi au cheo kilichokubalika) wa kuleta vitu vya kiroho (Baraka au laana) kutoka ulimwengu wa roho kuingiza katika ulimwengu wa mwili na kutoa vitu (sadaka/kafara/manuizio) kutoka katika ulimwengu wa mwili kwenda katika ulimwengu wa roho
a. Makuhani wa Jehova
Katika uliwengu wa nuru kuhani ni mtu yoyote aliyempokea Yesu na kuzishika amri zake (Ufunuo 5:10“ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.” Vilevile kuhani anaweza kuwa mtu yoyote aliyejifunza taratibu za kiibada yak i-Mungu kama mchungaji, shemasi, mwinjilisti, askofu, paroko n.k. mfano katika Biblia tunamuona Melkizedeki alikuwa kuhani wa Jehova.
Mwanzo 14:18 “Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana.”
b. Kuhani wa madhabahu za kishetani
Katika ulimwengu wa giza kuhani ni mtu yoyote ambaye anamtumikia shetani kwa kujua au bila kujua kwa lengo la kuleta uharibifu, nasema kwa kujua au bila kujua kwani kuna watu wanaitumikia mizimu ya nyumbani kwao wakidhani wanafanya kawaida kama walivyofanya baba na babu zao (mfano kuchinja kila mwaka, kuomba kwenye makaburi), lakini bila wao kujua kuwa wameshakabidhiwa ukuhani wa madhabahu za kishetani. Watu hawa huja kushtuka pale mambo yanapowaendea vibaya kwa kukiuka kanuni za kimadhabahu bila wao kujua. Mfano wa makuhani wa madhabahu za kishetani katika biblia ni makuhani wa dagoni na baali.
1 Samweli 5:5 “Kwa hiyo makuhani wa Dagoni, na mtu awaye yote aingiaye nyumbani mwa Dagoni, hawakanyagi kizingiti cha nyumba ya Dagoni huko Ashdodi, hata leo.”
1Wafalme 18:25-26 “25 Eliya akawaambia manabii wa Baali, Jichagulieni ng’ombe mmoja, mkamtengeze kwanza; maana ninyi ndio wengi; mkaliitie jina la mungu wenu, wala msitie moto chini. 26 Wakamtwaa yule ng’ombe waliyepewa, wakamtengeza, wakaliitia jina la Baali tangu asubuhi hata adhuhuri, wakisema, Ee Baali, utusikie. Lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu. Nao wakaruka-ruka juu ya madhabahu waliyoifanya.”
Kafara/sadaka ya madhabahu
Madhabahu haiwezi kukamilika kama hakuna kafara kwasababu kila mungu/Mungu wa madhabahu huhitaji kafara. Haijalishi uko upande gani lazima unapoenda madhabahuni uende na kafara/sadaka.
119 قسمت