DHAMIRA YA KUIFUTA ISRAEL KWENYE RAMANI YA DUNIA - Sehemu ya KWANZA
Manage episode 313499868 series 3273506
Katika karne ya 19 idadi kubwa ya Wayahudi waliishi katika maeneo kadhaa ya Milki ya Urusi yaliyotwaliwa na milki hiyo mnamo 1800.
Uadui dhidi ya Wayahudi ulitokea katika utawala wa Kirusi. Kuanzia mwaka 1880 kulitokea ghasia mbalimbali ambako Wayahudi walishambuliwa katika miji ya Urusi. Wimbi la pili la ghasia hizo zilizoitwa pogromu zilikatokea mwaka 1905, ambapo Wayahudi zaidi ya 2000 waliuawa mjini Odessa .
Wakati ule Wayahudi wa Urusi walianza kuhamia nje: wengi wao walikwenda Marekani, lakini wachache walielekea Palestina.
Mapogromu yalikuwa pia chanzo cha harakati mpya ya Uzayuni (Zionism) kati ya Wayahudi wa Ulaya. Uzayuni ulilenga kuwapa Wayahudi eneo maalum ili wapate kujenga upya taifa katika dola lao wenyewe, ambako wangekuwa wenyeji, si kundi la pekee katikati ya watu waliowadharau.
Mwaka 1896 Theodor Herzl (1860-1904) aliandika kitabu "Dola la Wayahudi" alimodai kuundwa dola la pekee kwa ajili ya Wayahudi. Mkutano wa kwanza wa wafuasi wake ulichagua jina la "zion" ambalo lilikuwa jina asilia la mlima wa hekalu mjini Yerusalemu; wakachagua jina hilo kwa sababu linataja mahali patakatifu zaidi pa Uyahudi.
Mkutano huo uliazimia kuwa "Uzayuni unalenga kuunda makazi salama yaliyokubaliwa rasmi kwa ajili ya taifa la Kiyahudi katika nchi ya Palestina".
Wazayuni walikusanya pesa kote Ulaya wakanunua ardhi katika Palestina na kuanzisha vijiji kwa ajili ya Wayahudi waliohima huko.
Palestina katika Milki ya Ottoman mwaka 1914
Vita ya Kwanza ya Dunia ilikwamisha mipango yote kwa sababu Palestina ilikuwa sehemu ya Milki ya Ottoman iliyoshiriki katika vita pamoja na Ujerumani na Austria dhidi ya Urusi, Ufaransa na Uingereza.
Mwaka 1917 wakati ambapo jeshi la Uingereza lilifaulu kusogea mbele kutoka Misri na kuingia Palestina, waziri wa mambo ya nje Arthur James Balfour alitoa tamko la Balfour yaani tamko rasmi kuwa Uingereza inataka kusaidia mipango ya kuanzisha makazi ya Kiyahudi katika Palestina. Wakati uleule Waingereza waliwaahidi Waarabu kuundwa kwa dola la Kiarabu kwenye maeneo yaliyokaliwa nao katika Milki ya Ottoman. Lakini wakati huohuo walipatana na Ufaransa kuhusu ugawaji wa maeneo ya Kiarabu ya Milki ya Ottoman.
119 قسمت